KUHUSU PANGISHA

KARIBU PANGISHA

Pangisha ni mfumo wa TEHAMA uliotengenezwa mwaka 2017 na vijana wa kitanzania waliopata changamoto za hapa na pale kipindi wanatafuta nyumba za kupanga.

KWANINI PANGISHA

Pangisha imetengenezwa kwa lengo la kurahisisha utafutaji wa nyumba za kupanga au za kununua bila kutumia muda mwingi au nguvu kazi kubwa kuulizia kwa watu na kuzunguka kutafuta nyumba. Pangisha inasaidia kuepukana na hizo changamoto haswa kwa mtu anayehitaji nyumba. Mfumo wa Pangisha unamsaidia mtafutaji kupata nyumba bora zenye mapendekezo yake binafsi kwa mfano sehemu anayotaka (mkoa gani au wilaya ipi), aina ya nyumba kama ni kwa ajili ya familia au kwa wanafunzi na pia ukubwa wa vyumba unazingatiwa.

Nyumba zinazopatikana kwenye mfumo wa Pangisha zinatangwaza na wamiliki wa nyumba na madalali walio maeneno mbalimbali nchi nzima. Uwepo wa ushirikiano baina ya watu hawa unachangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa nyumba kwenye mfumo Pangisha na vivyo hivyo upangishwaji wa nyumba hizo. Kama wewe ni mmiliki wa nyumba na ungependa kuipangisha basi unaweza kutumia tovuti yetu ili nyumba iweze kufahamika kwa wale wanaohitaji kupanga. Huu mfumo unapatikana wakati wowote na unaweza kuutumia popote kama umeunganishwa na mtandao wa intaneti kwenye kifaa chako cha kielektroniki ;). Pia tunapatikana mtandaoni muda wa kazi, kwahiyo ukihitaji msaada wa aina yoyote bila shaka tutakuwepo kukusikiliza.

Kutokana na uwepo wa nyumba za kupanga kwenye mfumo wa Pangisha zinazopatikana mikoa mbalimbali nchini Tanzania, una uwezekano mkubwa wa kupata nyumba ya kupanga kwenye mfumo huu kuliko sehemu ingine yoyote. Unasubiri nini? Tafuta nyumba yako mpya kwenye mfumo wa Pangisha.