Msaada

TAFUTA NYUMBA


Kuna maeneo mawili ya kisasa ya kutafuta nyumba, wewe kama mtafutaji, una uwezekano mkubwa wa kupata nyumba yenye sifa zinazoendana uchaguzi wako.

Sehemu ya kwanza ya kutafuta nyumba iko kwenye ukurasa wa mwanzo na ina vipengele vitano, cha kwanza ni cha mkoa, unaweza kuchagua mkoa tu na kisha kubonyeza kifungo cha "tafuta nyumba", na baada ya hapo, mfumo utakuonyesha nyumba zote kutoka mkoa huo. Ukishachagua mkoa kwenye kipengele cha kwanza, kipengele cha pili ambacho ni cha wilaya kitakuonyesha wilaya za mkoa uliochaguliwa awali. Kwa mfano kama mkoa uliochaguliwa ulikuwa ni Dar es Salaam, basi inamaanisha wilaya zitakuwa ni Ilala, Kinondoni na Temeke. Na ndivyo hivyo itatokea ukishachagua wilaya fulani, zitakuonyesha kata zake kwenye kipengele cha tatu na ukishachagua kata fulani, zitakuonyesha mitaa yake kwenye kipengele cha nne. Ukishamaliza kufanya machaguo yako basi bonyeza kifungo cha “tafuta nyumba” kupata nyumba zinazoendana na machaguo yako.

Sehemu ya pili ya kutafuta nyumba inategemea NENO maalum, neno linaweza kuwa eneo nyumba inakopatikana ambapo mtafutaji ataandika jina la mkoa au jina la wilaya au jina la kata au jina la mtaa. Pia anaweza kuandika bei ya kupanga nyumba au aina ya makazi anayohitaji, kama ni familia au kwa wanafunzi. Na pia kuna sifa ambazo nyumba inakuwa nazo kama uwepo wa jiko, kiyoyozi, maegesho ya gari, hapa mtafutaji atandika tu hilo neno na injini yetu ya kutafuta nyumba itampatia nyumba zinazoendana na neno ambalo ameliandika awali.


WAKALA


Wakala anaweza kuwa mmiliki wa nyumba au dalali, ndio wakuwasiliana nao wakati mtumiaji ameona nyumba inayofaa. Wakala wanaweza kuweka namba zao za simu hadi 3 kwa ajili ya kupata mawasiliano na anwani zao bila shaka.

Kama wakala, unatakiwa kujiandikisha kwanza uwe na akaunti yako ambapo utaweza kusimamia nyumba ulizoziongeza kwenye mfumo. Wakala anapaswa kubadilisha taaarifa za nyumba, kipengele cha hali ‘status’ pale nyumba inapopata mpangaji au kununuliwa ili mtumiaje asipate shida ya kuangalia nyumba iliyokwisha kupangishwa kwa wakati husika.


MAWASILIANO


Hapa unapata maelezo ya mawasiliano juu ya jinsi ya kutufikia sisi na na kuna fomu ya kujaza ambapo unaweza kutuwasilisha tatizo lake, swali au hata maoni kuhusu huduma yetu. Kama huna kompyuta au una shida yoyote, unaweza kutupata kwa kupitia namba zetu za simu +255 755 248731.